DP Ruto atifua kivumbi kaunti ya Meru, apinga BBI
- DP Ruto sasa amebadili msimamo na kusema kuwa anaielewa Deep State na System ambayo amekuwa akiteta kuhusu
- Alisema hakuna kitu ambacho kitamzuia kuingia Ikulu ifikapo 2022 Wakenya wakimpa kura
- DP alipuuza haja ya ripoti ya BBI akisema sasa ni wakati wa mjadala kuwa kuhusu Wakenya wa kawaida
Naibu Rais William Ruto ameanzisha kampeni za kupinga ripoti ya BBI ambayo inatarajiwa kuzinduliwa hivi karibuni na Rais Uhuru Kenyatta na Raila Odinga.
Akiwa kwenye ziara kaunti ya Meru, DP alisema mjadala umekuwa kuhusu mamlaka na vyeo na sasa wakati umefika viongozi wazungumzie masuala ya Wakenya walala hoi.
"Hatuwezi kuangazia BBI ambayo lengo lake ni kuunda nafasi nne za kazi kwa watu ambao tayari wana kazi na tusahau kuhusu ajenda nne za serikali ambapo ujenzi wa nyumba ulikuwa utengeneze nafasi za kazi milioni nne," alisema DP ruto.
Aliwataka viongozi wenzake kumaliza mjadala wa mamlaka na badala yake waanze kuzungumzia sera za kubadilisha maisha ya Wakenya.
Habari Nyingine: Aden Duale aomboleza baada ya ajali barabarani
"Kwa miaka mingi tumekuwa tukizungumzia vyeo. Tumeongea kuhusu wadhifa wa waziri mkuu na manaibu wake na nyadhifa zingine kubwa.
Ni wakati sasa mjadala uwe kuhusu vile tutabadilisha maishaya mwananchi wa kawaida," alisemaDP.
Habari Nyingine: Uwanja wa elimu kunapigwa Taekwondo kali sana
Wandani wake walifuata mkondo wake huku wakiwataka Wakenya kukataa ripoti ya BBI wakisema haimjali mwananchi wa kawaida.
"Hii BBI sisi tunaikataa. BBI tumeikataa, tumeikataa," Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa aliongoza nyimbo kukemea ripoti hiyo.
Aidha DP Ruto alisema alisema hakuna kitu au mtu ambaye atasimama kwenye barabara yake ya kuelekea Ikulu.
Habari Nyingine: Waziri Magoha hatukuelewi, sauti yako imejaa viraka leo hivi kesho vile jirekebishe
"Mnataka kuniambia kuwa mimi kama naibu rais sijui chochote kuhusu deep state? Nataka niwahakikishia kuwa tutakuwa ndani ya serikali ijayo," alisema katika eneo la Maua.
Ruto awali amekuwa akiteta kuwa kuna kundi la watu linaitwa deep state na system ambalo linapania kuhakikisha hajaingia Ikulu.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjbYJ4gpZmm6lloqrBsHnAraCfrZFiuKrC1KaZomWblsKvwMhmsJplnZq%2FtnnAqaCnn5Fir6O1jaGrpqQ%3D