Afisa wa DCI akamatwa kuhusiana na wizi wa mamilioni ya pesa
Polisi mjini Mombasa wanawazuia washukiwa watatu miongoni mwao akiwa afisa mmoja kutoka Idara ya Uchunguzi wa Uhalifu (DCI), kwa madai ya kuhusika katika wizi.
Mshukiwa huyo, Fadhil Masoud, ambaye ni konstebo kutoka Idara ya DCI ya Stesheni ya Polisi ya Railways, alikamatwa mnamo Ijumaa, Februari 14 asubuhi eneo la Nyali pamoja na wenzake.
Habari Nyingine: Wanafunzi wa darasa la kwanza wafika shuleni wakiwa walevi
Habari Nyingine: DCI wapekua afisi ya DP Ruto, wabeba kamera za CCTV
Kulingana na polisi, watatu hao walivamia magari mawili ambayo yalikuwa yanasafirisha pesa na kuiba zaidi ya shilingi milioni moja.
Kamanda wa polisi wa Mombasa, Eliud Monari, alisema washukiwa hao walikamatwa katika nyumba moja eneo la Nyali.
Habari Nyingine: Dereva afariki kwenye ajali mbaya Lang'ata
“Tuko na washukiwa watatu kizuizini na wako katika Kituo cha Polisi cha Central. Mmoja wa washukiwa ni afisa wetu kutoka idara ya upelelezi ya Kituo cha Polisi cha Railways” alisema kamanda huyo kama alivyonukuliwa na Nairobi News.
Duru zinaarifu kuwa kachero huyo wa DCI, ambaye anaaminika kuwa kiongozi wa genge hilo, amekuwa akikodisha magari na bunduki ambazo zimekuwa zikitumiwa na wenzake kutekeleza ujambazi.
Washukiwa wengine wawili wanatokea Nairobi na wanasemekana kuzuru Mombasa kila mara kutekeleza uhalifu pamoja na afisa huyo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690.
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjaX15fpBmmJ%2Bho5Z6uK2MnZqiZZGgrq6t07CYZqOlncK0tcCnmGamkWLEqsbIZq6aZZ2Wuqq4yKilomWplnqxsdKaZaGsnaE%3D