Mshahara wa Mkenya Victor Wanyama katika klabu ya Spurs waanikwa
Mishahara ya wachezaji wote wa Ligi Kuu Uingereza msimu huu imefichuliwa na shirika la Spotrac.com.
Katika ripoti hiyo, klabu ya Manchester United ndio hutumia hugharamika zaidi kuwalipa wachezaji wake wa timu ya kwanza mishahara yao huku mvamizi Alexis Sanchez akiwa miongoni mwa wachezaji wa kulipwa zaidi ugani Old Trafford licha ya kuwa kwenye safari ya kusajiliwa kama mchezaji wa mkopo wa mabingwa wa Serie A Inter Milan.
Mshahara wa Sanchez unazidi wa wachezaji wa Sheffield United ambao hulipwa pauni 14 milioni kila mwaka huku huyo wa United akitia kibindoni Euro 21 milioni kila mwaka.
Habari Nyingine: Mwanamuziki Rayvanny aanika tofauti zake na mkewe mtandaoni
Habari Nyingine: Harambee Starlets wabeba Kombe la Ceacafa 2019 kwa kumpiga bingwa mtetezi Tanzania 2-0
David de Gea ndiye mwanasoka anayelipwa zaidi Man United huku akitia kikapuni Euro 375,000 (KSh49milioni) kila wiki akifuatiwa na Sanchez ambaye hulipwa Euro 350,000 (KSh46milioni) kila wiki naye Paul Pogba akiwa watatu na Euro 290,000 (KSh38milioni) kila wiki.
Sogora Mkenya wa Tottenham Hotspur Victor Wanyama ambaye hupokea 3,380,000, hulipwa mshahara wa KSh436milioni kila mwaka.
Hii ina maana kwamba Wanyama hulipwa kitita cha pauni 65,000 (KSh8.3 milioni), kila wiki ambapo sasa nahodha huyo wa Harambee Stars anashikilia nafasi ya 14 katika orodha ya mishahara ya wachezaji wa Spurs
Habari Nyingine: Fundi wa kutikisa nyavu Michael Olunga afunga mabao 7 katika mechi moja
Mshambulizi mahiri wa Spurs, Harry Kane na kiungo wa kati Tanguy Ndombele ndio wachezaji ambao wanalipwa zaidi katika katika klabu hicho huku wawili hao wakiweka pochini Euro 200,000 (KSh26 milioni) kila wiki.
Pia katika orodha hiyo mpya, Mohamed Salah ndiye mchezaji wa gharama kubwa Liverpool ambako hulipwa kima cha pauni 200,000 (KSh26 milioni) kila wiki akifuatiwa na Roberto Firmino na Virgil Van Dijk wote wakipata Pauni 180,000 (Sh23 milioni) kila wiki.
Mabingwa wa Manchester City, Kevin De Bruyne na Raheem Sterling ndio wachezaji wakulipwa zaidi katika klabu hiyo ambapo hupokea Pauni 350,000 (KSh46milioni) na Euro 300,000 (KSh39milioni) kila wiki mtawalia huku Sergio Aguero akiwa wa tatu na Euro 230,135 (KSh30miloni) mshahara wa kila wiki.
Orodha ya Mishahara ya vilabu vya Ligi Kuu
Manchester City = £115,000
Liverpool =£100,000
Chelsea = £95,000
Arsenal = £92,000
Manchester United = £90,000
Tottenham Hotspur = £72,500
Everton = £65,000
West Ham United =£65,000
Crystal Palace = £55,000
Leicester City= £50,000
Southampton= £50,000
Newcastle United = £38,000
Wolverhampton Wanderers = £36,673
Bournemouth =£35,000
Burnley = £35,000
Watford = £30,000
Brighton & Hove Albion= £30,000
Aston Villa =£25,000
Norwich City =£12,000
Sheffield United = £9,000
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia news@tuko.co.ke au WhatsaApp: 0732482690
Subscribe to watch new videosChanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdjZ4N1hZhmpKygkZ2us62MsJhmpZuau7qtjK%2BgnKyfp3q4rc2ymKaZXaCutbXKmmSkpJGXwm7FwGaqqa2iqHq4rcCnoKSvkWO1tbnL