Mwanamke wa miaka 65 atafuta mpenzi kwa kutaka watu kutuma maombi
-Mwanamke mmoja kutoka Thailand ameweka bango nje ya boma lake kutangaza kuwa anahitaji mpenzi
-Bango hilo linawataka wanaotaka kumtumia ujumbe ili awape habari zaidi
-Njia yake maalum ya kutafuta mchumba imevutia vyombo vya habari vya imataifa
Mwanamke wa miaka 65 kutoka Thailand amegonga vichwa vya habari katika vyombo vya habari vya kimataifa kwa kuweka tangazo la kutafuta mchumba nje ya lango lake.
Habari Nyingine: Mwanamume aachiliwa baada ya miaka 23 gerezani kwa makosa ya kuwekelewa
Sompong Chomphuprapet, kutoka mkoa wa Ubon Ratchathani aliandika katika bango hilo kwamba alihitaji mpenzi na mwanamume anayetaka alihitaji kumpigia simu ili ampe habari zaidi.
Bango hilo limeandikwa, “Mwanamke wa miaka 65, anafuta mpenzi wa miaka 60-70, aliyestaafu lakini aliye na pensheni. Nina moyo msafi, mkweli na nimo katika hali nzuri ya afya. Kama unataka, wasiliana nami.”
Pakua APP mpya ya TUKO upate habari BURE
Wakati wa mahojiano, alisema hajawa na bahati kwa sababu ndoa zake mbili ziliishia talaka.
Mume wake wa kwanza alikuwa mlevi ilhali ndoa yake ya pili ilikaa kwa miaka 13.
Habari Nyingine: Akombe ndiye kiini cha kubatilishwa kwa ushindi wa Uhuru
Alisema, “Ninataka mwanamume mzuri. Kukaa pekee ni upweke mwingi na uchungu. Ninataka mwanamume aliyestaafu, ninataka upendo kamili, ninataka tuishi panoja mpaka tutenganishwe na kifo. Ikiwa kuna mtu atakayenitafuta, natatathmini ikiwa ni aina yangu."
Tayari amepata wanaume wawili wanaomtaka, lakini aliwakataa kwa sababu mmoja hakuwa na pensheni, na mwingine alikuwa na miaka 59 na pensheni yake ilikuwa haitoshi.
Habari Nyingine: Hakuna anayemudu gharama ya kufanya mapenzi nami-Huddah Monroe
Lakini hajakata tamaa na anatumainia kupata mtu hivi karibuni.
Read ENGLISH VERSION
Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke
Subscribe to watch new videosSubscribe to Tuko youtube channel to watch more interesting videos
Chanzo: TUKO.co.ke
ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiaoRzgJNmpLCZnpa6rLGMsJhmpZmWuKJ5lW5kmqyRm8K1rYymp56mqp56rMPAZqKurJGgrm7DwK2sZqOlqcKurYymmKilkp57qcDMpQ%3D%3D