NovaVib

Cheche za moto zashuhudiwa NTV baada ya mbunge wa Jubilee kutoboa ukweli mchungu kuhusu Raila

- Mbunge wa Jubilee wa eneo bunge la Tiaty Kasait Kamket anaamini kuwa hesabu ya kikabila Kenya katu haitawahi kuruhusu urais wa Raila Odinga

- Kasait ni mumewe Immaculate Kasait, mojawapo wa maafisa wa IEBC ambao NASA inataka wafurushwe kwa kuingilia uchaguzi ili kumpendelea Uhuru Kenyatta

- Olga Karani, naibu mmoja wa maafisa wa timu ya kampeni ya NASA alimweleza Kamket kumwambia mkewe ajiondoe ili upinzani uonyeshe jinsi utakavyoshinda uchaguzi Oktoba 26

Cheche za moto zilishuhudiwa wakati wa mahojiano ya televisheni katika NTV wakati Larry Madowo alimwalika Mbunge wa Jubilee Kasait Kamket na Olga Karani, mojawapo wa manaibu wa timu ya kampeni ya National Super Alliance.

Pakua APP mpya ya TUKO upate habari BURE!

Katika mahojiano hayo yaliyofanyika Jumapili, Oktoba 8, Kamket alisema haiwezekani kwa mujibu wa hisabati kwa kiongozi wa NASA Raila Odinga kuwa rais wa Kenya.

“Ni jambo lisilowezekana katika hesabu za kikabila Kenya kwamba Raila Odinga anaweza kuwa rais. Haiwezekani kamwe hata kwa kutumia mbinu gani. Kadri anavyowapoteza majenerali wake, wakati mamia ya majenerali wako wanahama kila uchao, anaweza vipi kuwa rais wakati hisabati za kikabila hazimpendelei tangu uchaguzi 2013?

Habari Nyingine: Jaji Mkuu Maraga anaongea lugha ya Raila-William Ruto

Habari Nyingine: Raila na NASA wamefilisikika, najua kwanini-Uhuru

“Hali itazorota zaidi tutakapofika katika uchaguzi wa Oktoba 26. Hivyo basi tarehe 26 itakuwa siku ya kustaafu kwake baada ya muda mrefu katika siasa,” alisema Kamket.

Hisia za Kamket hazikumwendea vyema Karani aliyemjibu vikali.

Ni muhimu kufahamu kuwa Kamket ni mumewe Immaculate Kasait, mojawapo wa maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ambao NASA inataka wafurushwe.

Habari Nyingine: Mbunge wa Jubilee ataka Raila anyang'anywe paspoti kabla ya marudio ya uchaguzi

Habari Nyingine: Jamaa awashangaza wengi baada ya kujiuzulu ili kumfanyia Raila kampeni za urais

Kasait ni Mkurugenzi wa Usajili wa Wapiga Kura.

“Anasema haiwezekani kwa mujibu wa hesabu ilhali wanazunguka kote wakifanya kampeni nasi tumetulia kwa sababu kura zetu zimeongezeka. Wakenya hawapendi uongo jinsi watu wanavyopenda kusema, ikiwa kweli unajua Raila hatashinda tena, unaweza kuanza kwa kumweleza mkeo katika IEBC ajiondoe kwa kuwa ndiye chanzo cha kura zetu kuibiwa?

“Akijiondoa pamoja na marafiki zake wote, tutawaonyesha jinsi tutakavyoshinda. Kwa hakika kwa sababu ya watoto wako binafsi anapaswa kuwa mtu wa kwanza kung’atuka.

Read ENGLISH VERSION

Una maoni? Una habari ambayo ungependa tuichapishe? Tuma ujumbe kwa mhariri: mwangi.muraguri@tuko.co.ke

Subscribe to watch new videos

Chanzo: TUKO.co.ke

ncG1vNJzZmijmajEorTIpaBnrKWgvG%2BvzmeinmdiaoFyfJZmmqGdk52ybsbAZqSorJ9ix6K%2Fx66frpyZrK5uutOvZJuZkZmubsXAZqSbrZ6csm7DwGahrpqZobKmecquq6ian5Z6trfWnqOiZZ2YtW%2B006aj

Aldo Pusey

Update: 2024-09-28